IQNA

Jinai za Israel

Israel imebomoa Majengo 44 ya Wapalestina katika kipindi cha wiki mbili

22:09 - September 18, 2022
Habari ID: 3475803
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, utawala ghasibu wa Israel umebomoa majengo 44 ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ikiwa ni muendelezo wa siasa zake za unyakuzi wa ardhi za Palestinakinyume cha sheria.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema mamlaka za Israel katika kipindi cha wiki mbili zimevamia na kubomoa majengo 44 ya Wapalestina katika eneo la al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na katika eneo C la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kisingizio cha "ukosefu" wa vibali vya ujenzi."

Ripoti hiyo ilisisitiza kuwa kati ya majengo 44, "takriban majengo 35 yapo eneo la Area C, 19 kati ya hayo yaliharibiwa bila ya onyo.

OCHA pia ilithibitisha kwamba utawala wa Israel ulibomoa nyumba 11 za Wapalestina kwa "sababu za adhabu" tangu mwanzo wa mwaka, ikilinganishwa na tatu za 2021 na saba za 2020.

Ikiashiria tabia ya utawala ghasibu wa Israel ya kuharibu nyumba za Wapalestina wanaodaiwa kuhusika na oparesheni dhidi ya Israel, ripoti hiyo imesisitiza kwamba "ubomoaji wa adhabu ni aina ya adhabu ya pamoja, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa."

Utawala wa Israel uliikalia kwa mabavu ardhi ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ikiwemo al-Quds Mashariki, katika vita vilivyoungwa mkono na nchi za Magharibi mwaka 1967.

Tangu pale eneo hilo likiwa na mamia ya makaazi haramu ambayo yamekuja kuwahifadhi mamia ya maelfu ya walowezi wa Israel.

Wapalestina wanataka Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa sehemu ya taifa huru la baadaye lenye al-Quds Mashariki kama mji mkuu wake.

3480532

Habari zinazohusiana
captcha