Kusitishwa kwa mapigano mara moja ni " jambo la dharura zaidi kuliko hapo awali", OHCHR ilisema Ijumaa.
Akizungumza kabla ya vita vya Gaza kutumia siku 100 Jumapili, Msemaji Liz Throssell alisisitiza haja ya wafanyakazi wa OHCHR kufikia maeneo yote ya Eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu.
Wiki 14 zimepita tangu utawala wa Israel uanze kampeni yake ya kikatili ya mauaji na uharibifu katika Ukanda wa Gaza. Zaidi ya Wapalestina ambapo 23,000 wameuawa hadi sasa, wengi wakiwa wanawake na watoto, huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia ikiwa ni pamoja na nyumba, hospitali, shule, sehemu za ibada, mifumo ya maji, na vifaa vya Umoja wa Mataifa. Idadi kubwa ya wakazi milioni 2.2 wa Gaza sasa wameyahama makazi yao.
Throssell alikumbusha kwamba Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk amerudia kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano "kukomesha mauaji na mateso ya kutisha, na kuruhusu utoaji wa haraka na ufanisi wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wanaokabiliwa na viwango vya kushangaza vya njaa na magonjwa,” na kuongeza kuwa “hili ni jambo la dharura zaidi kuliko wakati mwingine wowote.”
Akizungumzia mwenendo wa uhasama, alisema OHCHR wamesisitiza mara kwa mara namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyokaidi na kupiiza kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa za kibinadamu.
Throssell alilitaka jeshi la utawala wa Israel kuchukua hatua za haraka za kuwalinda raia, kwa kuzingatia sheria za kimataifa.
3486784