IQNA

Sekta ya Halal

Sekta ya Halal ni kati ya Sekta zinazopanuka kwa kasi zaidi d­­uniani

20:56 - January 26, 2024
Habari ID: 3478257
IQNA - Waziri wa Biashara wa Saudi Arabia Majid bin Abdullah Al-Qasabi amielezea sekta ya ‘Halal’ kama moja ya sekta zinazokua kwa kasi zaidi duniani.

Akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Halal la Makka, Al-Qasabi alibainisha umuhimu wa kushuhudia ushiriki wa ndani na nje ya nchi sambamba na kusainiwa kwa mikataba sita pembezoni mwa hafla hiyo. Kongamano hilo limefanyika kuanzia Januari 23-25.

Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Maonyesho cha Makka  unaendelea kwa siku tatu na ulijumuisha  mijadala ya jopo. Sekta ya Halal inahusiana an utoaji wa huduma na bidhaa kwa mujibu wa mafundisho ya duni tukufu ya Kiislamu.

Al-Qasabi alisema: "Sekta ya Halal inasimama kama mojawapo ya sekta zinazopanuka kwa kasi duniani kote. Kwa sasa, soko la chakula Halal lina thamani ya takriban $2.5 trilioni, na linatarajiwa kufikia $5.8 trilioni mwaka 2033.

Sekta ya kimataifa ya bidhaa Halal  iko tayari kwa mabadiliko ambayo hayajawahi kushuhudiwa, kama alivyosema Abdullah Saleh Kamel, rais wa Jumuiya ya Biashara na Maendeleo ya Kiislamu, wakati wa hafla hiyo hiyo.

Alisema kuwa hadhi ya bidhaa Halal imeinuliwa hadi kitovu cha maslahi ya kimataifa kupitia uanzishwaji wa Halal Products Development Co. na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma.

  "Hii ni mara ya kwanza ambapo tunapata habari kuhusu hazina ya utajiri wa serikali inayoanzisha kampuni maalum ya ukuzaji wa bidhaa za Halal. Kwa kweli, tunajivunia kuwa kampuni hii ni mshirika wa kimkakati wa kongamano," Kamel alisema.

Mpango huo unalenga kuendeleza tasnia ya halal duniani na kuendeleza mfumo muhimu na unaonyumbulika wa bidhaa za halal nchini Saudi Arabia.

Fawaz bin Talal Al-Harbi, mwenyekiti wa HPDC, alisisitiza kuongezeka kwa nia ya kimataifa ya bidhaa na huduma za Halal, na matumizi yanayotarajiwa ya watumiaji kufikia $ 5 trilioni katika miaka ijayo.

Al-Harbi alisisitiza kuwa kongamano hilo linalenga kuwezesha sekta ya halal inayoahidi kwa kushirikisha sekta ya kibinafsi, wasimamizi, na mamlaka za kisheria ili kutumia fursa nyingi katika uwanja huu.

Lengo ni kufungua upeo wa matumaini kwa vijana, kukuza kubadilishana maoni, kubadilishana utaalamu na uzoefu, na kuanzisha mbinu za hivi punde za maendeleo ya sekta hii.

Kongamano hilo lilijumuisha mada mbalimbali zinazohusu tasnia ya Halal na sekta zinazohusiana nayo, kongamano hili lilishuhudia ushiriki mkubwa kutoka nchi kama vile  Nigeria, Chad, Indonesia, Uturuki, Thailand, Brazil na Misri. Mataifa haya yalionyesha aina mbalimbali za bidhaa na huduma za chakula halali, zinazoakisi utofauti na utajiri wa soko la halal duniani.

Huku kukiwa na ripoti tofauti kuhusu ukubwa wa soko la halal duniani, Yousuf Khalawi, katibu mkuu wa Jumuiya ya Biashara na Maendeleo ya Kiislamu, alisema kuwa soko la vyakula na vinywaji Halal  linakadiriwa kuwa kati ya dola trilioni 2.2 hadi 2.8.

3486953

Kishikizo: halal sekta ya halal
captcha