IQNA

Shirika la Kutetea Haki za Mashia (SRW)

Hali ya Kiafya ya Sheikh Zakzaky ni mbaya mno

10:08 - August 13, 2016
Habari ID: 3470519
Hali ya kiafya ya kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria INM, Sheikh Ibrahim Zakzaky inazidi kuwa mbaya, Shirika la Kutetea Haki za Waislamu wa Madhehebu ya Shia, SRW, limesema.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, SRW yenye makao yake Washington DC, Marekani imebainisha wasiwasi wake kutokana na hali mbaya ya kiafya ya Sheikh Zakzaky.

Katika taarifa SRW imesema hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inazidi kuwa mbaya kutokana na serikali kumpuuza pamoja na kuwa inamshikilia kwa zaidi ya miezi minane pasina kumfungulia mashtaka.

Shirika la Kutetea Haki za Waislamu wa Madhehebu ya Shia limeonya kuwa iwpao Sheikh Zakzaky hatapata matibabu ya harakat, basi yamkini akaaga dunia.

Halikadhalika SRW imetoa wito kwa serikali ya Nigeria kumuachilia huru mara moja Sheikh Zakzaky na Waislamu wengine wa madhehebu ya Shia waliokamatwa kiholela na kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.

Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Disemba mwaka jana 2015, siku moja baada ya jeshi la Nigeria kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waislamu katika mji wa ZariaIkumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.

Aidha Jeshi la Nigeria lilimkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake. Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inaripotiwa kuwa mbaya huku taarifa zikisema amepoteza jicho moja mbali na majeraha mengine mwilini. Serikali ya Nigeria inamshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu tokea Desemba mwaka jana pasina kumfungulia mashtaka.

3522050

captcha