IQNA

Serikali ya Kano, Nigeria yapiga marufuku Harakati ya Kiislamu

14:54 - October 08, 2016
Habari ID: 3470605
Katika muendelezo wa ukandamizaji wa Waislamu nchini Nigeria, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky imepigwa marufuku katika jimbo la Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, serikali ya Jimbo la Kaduna imeonya kuwa, yeyeote atakayepatikana kuwa mwanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria atafungwa jela miaka saba au atatozwa faini au yote mawili kwa pamoja.

Aidha serikali ya Kaduna imedai kuwa, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambayo aghalabu ya wanachama wake ni Waislamu wa madhehebu ya Shia wanashiriki katika maandamano yasiyo na kibali na kuzuia magari barabarani tangu Desemba mwaka jana.

Ikumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.

Aidha Jeshi la Nigeria lilimkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake. Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inaripotiwa kuwa mbaya huku taarifa zikisema amepoteza jicho moja mbali na kuwa na majeraha mengine mwilini. Serikali ya Nigeria inamshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu tokea Desemba mwaka jana bila kumfungulia mashtaka.

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu IHRCyenye makao yake Uingereza imeshapeleka faili la mauaji ya Waislamu katika mji wa Zaria katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague nchini Uholanzi.

Mwezi Machi IHRC ilisema faili la mashambulizi na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa mji wa Zaria limepelekwa Hague katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). 

3536361

captcha