IQNA

Umoja wa Waislamu

Kiongozi wa Ansarullah Yemen aonya kuhusu njama za Wazayuni za kuvuruga umoja wa Waislamu

21:57 - September 27, 2023
Habari ID: 3477660
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, Harakati ya Lobi ya Kiyahudi ya Kizayuni duniani pamoja na washirika wake inataka kupenya na kuwa na ushawishi baina ya Waislamu na hivyo kuudhibiti Umma wa Kiislamu.

Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa sherehe za Maulidi ya Mtume (SAW) na kueleza kwamba, uingiliaji wa maadui ni mkubwa na umefikia kiasi kwamba wameingilia hata mbinu za masomo za nchi za Kiislamu na Kiarabu kama vile Saudi Arabia na kuondoa Aya za Qur'ani kwenye vitabu vya kiada kwa sababu Mayahudi wamekasirishwa sana na aya hizi.

Akizungumzia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume (SAW), kiongozi huyo wa Ansarullah ya Yemen amesema, watu wa Yemen wanaadhimisha Maulidi kwa kuzingatia umuhimu na ukubwa wake kwa sababu ni moja ya hafla kubwa.

Amesema: Rasilimali za watu wa Yemen zimeporwa kwa miongo kadhaa na hazijatumika kuwahudumia wananchi, na viongozi wameahidi tu kuzitumia kwa manufaa ya wananchi.

Baadhi ya maofisa wa serikali ya zamani wanamwaga machozi ya mamba kwa uwongo kwa ajili ya watu wa Yemen, lakini wakati huo huo wako katika safu ya adui na wanachangia katika kumwaga damu za watu wa nchi hii.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake al-Houthi amezungumzia suala la uvamizi wa muungano wa Saudia huko Yemen na kusema: Taifa letu linakabiliwa na uvamizi ambao umekuwa ukifanya mauaji, uharibifu, mzingiro na kukaliwa kwa mabavu nchi hii. Kipaumbele muhimu zaidi cha taifa letu ni kukabiliana na hujuma na hakukuwa na ilibakia kidogo tu Yemen igeuke na kuwa nchi iliyo chini ya uvamizi wa kigeni.

3485329

Habari zinazohusiana
captcha