IQNA

Harakati za Qur'ani

Kijana wa Kipalestina asambaza Qur’ani Tukufu miongoni mwa wakimbizi huko Gaza

20:37 - January 25, 2024
Habari ID: 3478253
IQNA - Kijana wa Kipalestina amezindua mpango wa kusambaza nakala za Qur’ani Tukufu miongoni mwa wale wanaoishi katika kambi za wakimbizi katika eneo la Gaza ambalo linakabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wanam Badwan wanasema anatumai kuwa hatua hii itawasaidia wakimbizi kusoma Qur’ani nzima kama njia ya kutuliza huzuni yao.

Alisema watu wa Ukanda wa Gaza wamesahauliwa na ulimwengu na hawana njia nyingine zaidi ya kukimbilia Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ameiambia televisheni ya Al Jazeera.

Kwa mujibu wa Badwan, wengi wa raia wa Gaza waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi za wakimbizi hawana nakala za Qur’ani kwani wameacha nyuma kila kitu walichokuwa nacho.

Kutumia nakala za kielektroniki za Qur’ani Tukufu sio chaguo pia kwani muunganisho wa mtandao umekatika katika eneo hilo, alibainisha.

Wakimbizi hao wamekaribisha hatua hiyo. Hassan, ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi, aliielezea Qur’ani kuwa chemchemi ya nyoyo na akahimiza kila mtu kukisoma Kitabu hicho kitukufu na kufanyia kazi mafundisho yake.

Wakati uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza ukiendelea, Wapalestina wameendeleza shughuli za Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani na kusoma kozi kwenye mahema katika kambi za wakimbizi.

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Israel katika Ukanda wa Gaza yaliyoanza tarehe 7 Oktoba yamesababisha vifo vya takriban watu 26,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine zaidi ya 62,000.

Pia Wazayuni makaatili wameharibu maelfu ya nyumba pamoja na shule, hospitali, misikiti na makanisa na kusababisha idadi kubwa ya wakaazi wa Gaza kuyahama makazi yao.

3486948

Habari zinazohusiana
captcha