IQNA

UNICEF

Jeshi la Myanmar linatekeleza jinai dhidi ya watoto Waislamu

18:13 - November 11, 2016
Habari ID: 3470667
IQNA-Shirika la Umoja la Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF limebaini wasi wasiwake kuhusu jinai za kutisha dhidi ya watoto zinazotekelezwa na jeshi la Myanmar katika jimbo la Rakhine.

Taarifa ya UNICEF imesema kuwa, mwenendo wa wanajeshi wa kuwashambulia watoto wadogo wa Rohingya kaskazini mwa jimbo la Rakhine ni wa kutisha na kwamba taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imepokea ripoti za kunajisiwa na kudhalilishwa watoto wadogo katika eneo hilo.

Tangu Oktoba 9, eneo hilo limekuwa chini ya mzingiro wa maafisa usalama wa Myanmar, baada ya kuuawa maafisa tisa wa polisi; mauaji ambayo serikali inadai yalitekelezwa na Waislamu wa kabila la Rohingya.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema maafisa usalama katika eneo hilo mbali na kutekeleza mauaji dhidi ya Waislamu walio wachache, lakini pia wanawabaka wanawake na mabinti wadogo sambamba na kuwasweka mbaroni Waislamu wasio na hatia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraiaWaislamu ambao idadi yaoni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesiakutokana na mashambulio ya mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.../

captcha