IQNA

Diplomasia

Naibu Mkuu wa Hizbullah: Mapatano ya Iran na Saudi Arabia ni hatua ya kishujaa

14:05 - April 20, 2023
Habari ID: 3476893
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya Iran na Saudi Arabia ya kuanzisha tena uhusiano wao wa kidiplomasia yalikuwa ya kishujaa.

Sheikh Naim Qassim sambamba na kuashiria kwamba, hivi sasa eneo la Asia Magharibi linaelekea upande wa amani na uthabiti ameyasifu makubaliano ya Iran na Saudia yaliyofikiwa kwa upatanishi wa China.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameisifu hatua hiyo ya Iran na Saudia na kubainisha kwamba, makubaliano hayo yamefikiwa kwa kuwa Riyadh na Tehran zinataka kushirikiana baina yao na kuweka muongozo wao kwa ajili ya kuleta uthabiti wa kisiasa wa nchi zao na eneo hili la Asia Magharibi.

Aidha ameongeza kuwa, kile kilichofikiwa baina ya Iran na Saudia kimebadilisha muelekeo wa Asia Magharibi na kwa mara nyingine tena utawala haramu wa Israel umekuwa adui wa kweli wa watu wote.

4135528

captcha