IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu

Msomi: Marekani, Israel 'zimeshangazwa' na mapatano ya Iran-Saudi

17:59 - March 12, 2023
Habari ID: 3476698
TEHRAN (IQNA)-Mhadhiri mwenye makao yake nchini Uingereza anasema Washington na Tel Aviv "zilishangazwa" baada ya Tehran na Riyadh kutangaza kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia siku ya Ijumaa.

Nchi hizo mbili za Kiislamu zilikubaliana kurejesha uhusiano na kufungua tena balozi baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo yaliyopatanishwa nchini Iraq pamoja na siku za mazungumzo makali yaliyopatanishwa na China. Maelewano hayo yanakuja miaka saba baada ya mataifa hayo mawili kukata uhusiano kutokana na masuala kadhaa.

Ili kujadili zaidi maendeleo na athari zake za kikanda,  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)  imewasiliana na Stephen Chan, profesa wa siasa za dunia na uhusiano wa kimataifa katika SOAS, Chuo Kikuu cha London. Amechapisha vitabu kadhaa kuhusu mahusiano ya kimataifa na makala pamoja na hakiki katika vyombo vya habari vya kitaaluma

Haya hapa mahojiano hayo:

IQNA: Kwa maoni yako, mapatano ya Iran na Saudi Arabia yatakuwa na taathira gani katika eneo la Mashariki ya Kati, hususan katika vita vya Yemen?

Chan: Mafanikio  hayo ya kidiplomasia yatakuwa na athari chanya katika eneo lote, sio tu kwa sababu ya ushirikiano wa kidiplomasia lakini kile ambacho maelewano hayo yanaweza kufanikisha.

Walakini, hakuna kitu kinachopaswa kuzingatiwa kuwa kiotomatiki. Vita nchini Yemen, kwa mfano, vinahusisha pande mbili ambazo hazipaswi kuonekana kama wateja tu. Wana ajenda kali na sababu zao wenyewe. Kwa hivyo, ingawa sasa kunaweza kuwa na uwezekano wa mazungumzo, kuna uwezekano kwamba mazungumzo yatakuwa ya muda mrefu na magumu.

IQNA: Je, unadhani kuna kikwazo gani kikubwa katika kupatikana kwa amani nchini Yemen?

Chan: Pande zote mbili nchini Yemen zina silaha za kutosha. Hakuna upande utakaotamani kuacha mafanikio yoyote kwenye uwanja wa vita ambao unafikiri wameshinda. Kutakuwa na haja ya kuwa na kikosi cha kulinda amani na ufuatiliaji kuwekwa na ni vigumu sana kuhakikisha ni nchi gani inaweza kuonekana kama neutral kutosha kuchangia askari wa kulinda amani. Na itawabidi wawe askari wenye uwezo wa hali ya juu wa kupambana kwani usitishaji mapigano wowote ule unaokubaliwa ungekuwa rahisi kuvunjika na, kama si vinginevyo, kikosi cha kulinda amani kinaweza kushikwa na mapigano makali.

IQNA: Je, unadhani kuanzishwa tena mahusiano kati ya Tehran na Riyadh kuna athari gani kwa ushawishi wa Marekani na Israel katika eneo la Mashariki ya Kati?

Chan: Marekani na Israel zilishangazwa na mapatano hayo. Israel ilikuwa ikitegemea kuendelea uadui wa Saudia na. Zaidi ya yote, Israel haitaki Iran yenye uwezo wa kukabiliana nayo. Wasaudi walijua kuwa walikuwa wakiifaidisha Israel katika uadui wao dhidi ya Iran.

Kwa upande wa Marekani, haikufikiria kamwe Wachina wanaweza kufanikisha mafanikio kama haya. China sasa ni nchi yenye ushawishi wa kidiplomasia katika Mashariki ya Kati.

IQNA: Je, inaweza kusemwa kwamba ukuruba wa Iran na Saudia ni ishara ya kushindwa Israel kuanzisha uhusiano wa kawaida na Riyadh?

Chan: Israel iliitazama Saudi Arabia kama  kama mshirika muhimu dhidi ya Iran. Israel haikuwahi kuthamini ushawishi wa Saudi Arabia katika uhusiano wa kimataifa. Kwa hiyo Israel haikuwahi kuwa na uhusiano mpana Saudi Arabia zaidi ya mtazamo finyu sana. Tel Aviv inatazama ulimwengu kupitia tu lenzi yake ya ubinafsi.

IQNA: Je, makubaliano yatakuwa na athari gani katika mliangano wa nguvu katika Mashariki ya Kati?

Chan: Mapatano hayo yanaifanya Qatar kuwa na umuhimu mdogo kama njia ya kidiplomasia kati ya maslahi ya Sunni na Shi'a, kwani mkondo wa kidiplomasia unaweza sasa kuwa wa moja kwa moja - ingawa hautakosa changamoto.

Mabadiliko makubwa katika mlingano wa madaraka yatakuwa katika athari kwenye mahesabu Israel. Lakini kuna uwezekano pia kuwa na athari katika mtazamo wa Misri kwa Hamas. Kimsingi mabadiliko mengi yatajiri.

IQNA: Baadhi wanaamini kwamba hatua hii ni utangulizi wa matukio muhimu zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. Je, unadhani ni tukio gani litakalofuata lenye ushawishi mkubwa katika eneo hili?

Chan: Ni nini kitakachofuata hakiwezi kutabiriwa sasa hivi. Kiwango uhusiano wa kibalozi kila pande kitakuwa muhimu.

Napoleon alisema kuwa ulimwengu unapaswa kuwa mwangalifu ikiwa China itaamka. Madola ya Magharibi yanaamini ni Iran ambayo sasa haipaswi kuruhusiwa kuamka. Kwa hivyo ni muhimu sana Iran iwe na uangalifu kuhusu namna inavyojidhihirisha ulimwenguni.

captcha