IQNA

Mbunge Mwislamu adhalilishwa Marekani baada ya kuondoka White House

14:17 - December 08, 2016
Habari ID: 3470724
IQNA- Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomali kuchaguliwa nchini Marekani amemdhalilisha na dereva wa teksi ambaye amemtusi kwa maneno ya chuki dhidi ya Uislamu mjini Washington.

IQNA- Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomali kuchaguliwa nchini Marekani amemdhalilisha na dereva wa teksi ambaye amemtusi kwa maneno ya chuki dhidi ya Uislamu mjini Washington.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ilhan Omar, ambaye aliwahi kuwa mkimbizi nchini Marekani na ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Minnesota katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita, amechapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa: "Nilipokuwa nikiondoka kwenye mkutano wa sera katika Ikulu ya White House nikielekea hotelini, nilikumbana na tukio la kibaguzi na chuki ambalo sijawahi kulishuhudia tena. Dereva wangu wa teksi alianza kunitolea maneno ya chuki na kuniita mfuasi wa kundi la kigaidi la ISIS huku akitishia kunivua hijabu."

Mtunga sheria huyo wa Kisomali ameongeza kuwa: "Sielewi watu wanatoa wapi ujasiri wa kueneza wazi wazi chuki zao dhidi ya Waislamu."

Kumejiri matukio kadhaa ya kushambuliwa wanawake Waislamu waliokuwa wamevaa vazi la stara la Hijabu huku maandishi ya kibaguzi yakiandikwa katika misikiti.

Kwa mujibu Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR), ambalo hutetea haki za Waislamu, mbali na wanawake Waislamu kushambuliwa pia kumeshuhudiwa hujuma dhidi ya watoto Waislamu.

"Hii ni natija ya chuki dhidi ya Uislamu kuwa sera rasmi kama ambavyo tumeshuhudia miezi ya hivi karibuni katika kampeni za uchaguzi wa rais,” amesema msemaji wa CAIR Ibrahim Hooper. Aidha amesema ni jukumu la Trump kulaani ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu. Hadi sasa Trump au wapambe wake hawajatoa taarifa yoyote kuhusu kuongezeka hujuma dhidi ya Waislamu Marekani.

Ilhan Omar mwenye umri wa miaka 33 alizaliwa Somalia kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vita katika nchi yake.

Alipokimbia Somalia awali aliishi kwa muda wa miaka mine katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya kabla ya kuelekea Marekani katika eneo lenye Wasomali wengi la Cedar-Riverside ambapo aliishi kwa miongo miwili na sasa ni mkurugenzi wa Jumuiya ya Kuwaleta Pamoja Wanawake.

3552185

captcha