IQNA – Saudi Arabia imewafukuza raia wa kigeni wasiopungua 8,000 kama sehemu ya kampeni ya usalama kwa lengo la kuhakikisha utaratibu kabla ya Hija ya mwaka huu, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza.
IQNA – Mkutano wa Kimataifa kuhusu "Haki za Binadamu kwa Mtazamo wa Mashariki" unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Aprili, 2025, jijini Tehran, na utaendelea tarehe 28 na 29 Aprili katika Chuo Kikuu cha Baqir al-Olum mjini Qom.
IQNA – Baadhi ya mashekhe wakubwa wa Qur’ani kutoka Misri wametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Abdolrasoul Abaei, mtaalamu mashuhuri wa Qur’ani nchini Iran.
IQNA – Uchunguzi wa kina kuhusu hali ya hati za Kiarabu na Kiislamu zipatazo 40,000 katika maktaba tatu kubwa zaidi za umma nchini Ujerumani umefichua nukta za kuvutia kuhusu uhusiano wenye sura nyingi kati ya Ulaya, Mashariki ya Kati, na Afrika Kaskazini.
IQNA- Kikao cha kumi na nne cha kila wiki cha Tafsiri ya Qur'anI katika Msikiti wa Al-Azhar nchini Misri kitafanyika kwa mada "Msikiti wa Al-Aqsa katika Quran".
IQNA – Kongamano lililopewa jina “Jinsi ya kutumia Akili Mnemba (Artificial Intelligence-AI-) kuhudumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kuwasaidia Ndugu Zetu wa al-Quds” iliandaliwa nchini Mauritania.
IQNA – Kadri maandalizi ya Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamu yanavyoendelea, tarehe ya mwisho kwa washiriki wa sehemu ya Teknolojia na Ubunifu Kuhusu Qur’ani inakaribia.
IQNA – Baadhi ya watu humkumbuka Mwenyezi Mungu pale tu wanapojiridhisha kuwa njia zote zimefungwa. Ni pale wanapoona kuwa kila njia imezibwa ndipo huamua kumtegemea Mwenyezi Mungu.
IQNA – Watu wa Tunisia wamefanya maandamano katika mji mkuu Tunis na miji mingine siku ya Ijumaa, wakitaka kuwekwa sheria ya kuzuia uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.
IQNA-Msikiti wa UKIM Sparkbrook Islamic Centre huko Birmingham, Uingereza, umesifiwa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Birmingham kukusanya tani 120 za taka.
IQNA-Umoja wa Mataifa umesema wanawake na watoto wa Kipalestina ndio pekee waliouawa katika mashambulizi yapatayo 36 ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza tangu katikati ya mwezi Machi na kuonya kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Israel yanahatarisha "kuendelea kuwepo Wapalestina kama jamii".
IQNA-Haj Ryoichi Umar Mita alikuwa mfafsiri wa kwanza wa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kijapani. Alizaliwa mwaka 1892 katika mji wa Shimonoseki, Mkoa wa Yamaguchi, kisiwa cha Kyushu, Japan, katika familia ya Kisamurai na Kibuddha.
KARAJ (IQNA)- Tamasha Maua ya Tulip limeanza April 4, 2025 katika mji wa Karaj, mkoa wa Alborz magharibi mwa Tehran nchini Iran. Tamasha hilo linafanyika katika Bustani ya Chamran na kuna maua zaidi ya 150,000 ya Tulip ya rangi mbali mbali.
IQNA – Waislamu nchini Singapore (Singapuri) wamejitolea kuchangia nyama kwa watu wa Gaza wakati wa sikukuu ya Idul Adha, kutokana na janga la kibinadamu katika Ukanda huo uliozingirwa na utawala dhalimu wa Israel.